Ripoti ya Wikileaks kinyume na sheria

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington, imesema uchapishaji wa maelfu ya nyaraka za siri unaoatarajiwa kufanywa na tovuti iliyobobea kutoboa siri, Wikileaks ni kinyume na sheria za Marekani.

Image caption Marekani yaonya madhara ya ripoti ya Wikileaks

Onyo hilo lilitolewa katika barua ambayo mshauri wa masuala ya sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Harold Koh, alimwandikia mwanzilishi na mmiliki wa tovuti hiyo, Julian Assange.

Barua hiyo ilitumwa siku moja baada ya Marekani kuonya maisha ya watu wengi yatakuwa hatarini ikiwa uchapishaji huo utafanyika.