Kenya yachemsha Cecafa

Matumaini ya Kenya kuingia katika raundi ya pili ya michuano ya Cecafa yaliingia dosari kubwa siku ya Alhamisi, baada ya kuchapwa 2-1 na Ethiopia.

Mchezo huo ulifuatiwa na mechi ya kusisimua kati ya Malawi na Uganda zilizotoka sare ya 1-1 kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Kenya na Ethiopia zilijitupa uwanjani zikiwa zimefungwa katika michezo yake ya ufunguzi siku ya Jumatatu.

Harambee Stars walifungwa 3-2 na Malawi, huku Ethiopia ikichapwa 2-1 na mabingwa watetezi Uganda.