Arsenal yarejea kileleni

Mabao mawili maridadi ya Samir Nasri yameipeleka Arsenal tena kileleni baada ya kupata ushindi dhidi ya Fulham. Arsenal imeshinda kwa magoli 2-1. Goli la Fulmah limefungwa na Diomansy Kamara.

Image caption magoli maridadi ya Nasri

Tottenham licha ya kuongoza kwa muda ikiwa ugenini, imetoka sare dhidi ya Birmingham City, kwenye uwanja wa St. Andrews. Sebastian Bassong ndio alifunga bao la Spurs katika dakika ya 19, huku bao la kusawazisha la Birmingham City likifungwa na Craig Gardner dakika ya 81.

Blackburn Rovers imeiachia kisago Wolves kwa mabao 3-0. Davin Dunn, Brett Emerton na Ryan Nelsen wakifunga mabao hayo.

Chelsea imeendelea kujivuta baada ya kutoka sare ya 1-1 na Everton. Didier Drogba alifunga bao la Chelsea kwa njia ya mkwaju wa penati dakika tatu kabla ya mapumziko, huku bao la kusawazisha la Everton likifungwa na Jermaine Beckford katika dakika ya 86.

Image caption Carlo Ancellotti

Nahodha wa Manchester City Carlos Tevez ameongoza kwa mfano, baada ya kuipatika timu yake bao pekee na la ushindi dhidi ya Bolton.

Na katika mchezo mwingine, Wigan imetoka sare ya 1-1 na Wigan. Mabao ya Wigan yamefungwa na Danny Collins wa Stoke aliyejifunga, na la pili Tom Cleverly. Magoli ya Stoke yamefungwa na Robert Huth na Matthew Ethrington.

Mchezo kati ya Blackpool dhidi ya Manchester United umeahirishwa kutokana na hali mbaya ya hewa kuathiri uwanja.