Kenya: Waislamu hawakuhusika kuua

Jeshi la polisi nchini Kenya limesema makundi ya Kiislam yenye itikadi kali, hayaku-husika katika mashambulio ya mabomu kwenye mitaa ya Nairobi, ambapo askari polisi watatu waliuwawa.

Image caption Nairobi baada ya shambulio

Kamanda wa polisi Matthew Iteere alisema haamini kuwa kundi Al-Shabab la Somalia lilihusika katika mashambulio ya siku ya Ijumaa.

Alisema huenda waliofanya maovu hayo ni gengi la wahalifu, ambao baadhi yao wanaoshukiwa, waliandamwa na kuuwawa.

Kenya imeitaka idara ya upelelezi ya Marekani, FBI, isaidie katika uchunguzi, ili kuwakamata wahusika.