Ivory Coast: Urusi yaweka vizingiti

Image caption Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice. Amesisitiza umoja huo una haki ya kumwidhinisha bwana Ouattara.

Mabalozi katika umoja wa mataifa wamesema Urusi inazuia kutolewa azimio la baraza la usalama la umoja huo litakalomwidhinisha kiongozi wa upinzani nchini Ivory Coast, Alassane Ouattara, kama rais mpya wa taifa hilo.

Image caption Hali ni tete nchini Ivory Coast.

Urusi imeelezea wasiwasi kwamba kwa kumtangaza bwana Ouatarra mshindi wa uchaguzi huo uliokumbwa na utata, umoja wa mataifa utakuwa umezidisha majukumu yake.

Hata hivyo balozi wa marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice amesema mkataba wa amani uliotiwa saini baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ivory Coast mwaka 2002 ulitoa uwezo kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo kuidhinisha uchaguzi wa urais.

Hapo awali jumuiya ya kiuchumi kwa mataifa ya Afrika magaribi, ECOWAS, iliondoa uanachama wa Ivory Coast kutokana na hatua ya rais wa sasa, Laurent Gbagbo kukataa kukubali kuwa alishindwa katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.