Tarakimu zaonyesha NDP yanawiri Misri

Image caption Kiongozi wa Upinzani nchini Misri Ayman Nuru awapungia mkono wafuasi wake katika kituo cha kupigia kura

Tarakimu rasmi zilizochapishwa nchini Misri zinaonyesha kuwa chama tawala cha NDP chake rais Hosni Mubarak kilishinda takriban asilimia themanini ya viti vyote vya ubunge katika uchaguzi uliofanyika hivi maajuzi.

Vyama viwili vikuu vya upinzani Muslim Brotherhood na Wafd, vilisusia duru ya pili ya uchaguzi huo iliyofanyika siku ya jumapili vikidai udanganyifu mkubwa ulifanyika katika duru ya kwanza.

Marekani na umoja wa Ulaya pia zimekosoa vikali jinsi uchaguzi huo ulivyoandaliwa lakini waziri mkuu wa Misri, Ahmed Nazif, amekanusha madai kuwa serikali iliingilia maandalizi ya uchaguzi huo.