Mfumo wa malipo Wikileaks wasimamishwa

Malipo ya mtandao wa Wikileaks kwa kutumia mfumo wa kadi maarufu kama Visa umesimamishwa.

Image caption Malipo kwa Wikileaks yasimamishwa

Uchunguzi utafanywa kuhusiana na jinsi shirika la Wikileaks linavyoendeleza shughuli zake.

Kampuni nyingine ya malipo, PayPal, imekatiza uhusiano wake na Wikileaks.

Wachambuzi wanasema hatua kama hizi zitazuia mtandao wa Wikileaks kufanya shughuli zake, kwa sababu unategemea sana ufadhili kutoka kwa wanaouunga mkono mtandao huo.

Siku ya Jumatatu serikali ya Uswizi ilifunga akaunti ya benki inayomilikiwa na muasisi wa Wikileaks, Julian Assange.