ElBaradei kuviunganisha vyama Misri

Mwanasiasa anayeongoza harakati za kuleta mabadiliko ya kimemokrasi nchini Misri, Mohamed ElBaradei, anasema anataka kuunganisha vikundi vya upinzani, ili viwe na nguvu dhidi ya chama tawala cha National Democratic cha Rais Mubarak.

Image caption Mohamed ElBaradei

Bwana ElBaradei ameliambia shirika la habari la AP, kwa vile upinzani umegawanyika, unashindwa kufanya maandamano makubwa.

Kiongozi huyo wa upinzani, aliyewahi kuwa mkuu wa shirika la Atomiki la Umoja wa Mataifa, aliwasihi wananchi wa Misri waungane, baada ya upinzani kushindwa vibaya katika uchaguzi wa wabunge mwezi uliopita.