Makampuni ya Marekani yatishiwa Zimbabwe

Makampuni ya ulaya na Marekani yanayoendesha shughuli Zimbabwe yanakabiliwa na tishio la kuchukuliwa hatua na serikali, iwapo vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa hilo, havitaondolewa.

Image caption Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Katika hotuba kali kwenye mkutano wa chama chake cha Zanu PF, mjini Mutare, Rais Robert Mugabe, amesema wakati umefika kulipiza kisasi dhidi ya jamii ya kimataifa, kwa hatua ambazo zinaumiza watu wake.

Rais Mugabe alitarajiwa pia kuhudhuria tamasha la muziki la vijana.