Baridi yazidi kuleta kizaazaa michezoni

Hali ya hewa ya baridi kali inaendelea kuleta bugudha kubwa katika michezo nchini Uingereza, hasa wakati huu wa sikukuu.

Image caption Uwanja kama huu hauchezeki kwa theluji

Michezo ya Ligi Kuu ya soka ya England kati ya Blackpool na Liverpool na kati ya Everton na Birmingham imefutwa.

Ipswich ambao walikuwa wawakaribishe nyumbani Watford katika mechi za Championship, mchezo huo nao umeahirishwa, wakati mechi ya Ligi Kuu ya Scotland kati ya Kilmarnock na Dundee United nao umeahirishwa.

Michezo ya rugby, pambano baina ya Gloucester na Northampton limeahirishwa kutokana na baridi kali.

Pia michezo mingine ya rugby ya ligi kuu kati ya Bath na Exeter umefutwa na ule baina ya Newcastle dhidi ya Leeds umesogezwa mbele, badala ya kufanyika Jumapili, sasa utachezwa Jumatatu.

Katika soka tena, michezo ya Championship ya Crystal Palace, Derby, Ipswich, Scunthorpe na Middlesbrough pia imefutwa; michezo 22 ya Ligi daraja la kwanza na la pili pia imeahirishwa.

Mechi ya ligi daraja la kwanza pekee itakayochezwa ni kati ya Huddersfield na Hartlepool, wakati ya ligi daraja la pili, kati ya Wycombe na Hereford umenusurika na utachezwa kama ilivyopangwais the