Makundi ya wanamgambo kuungana Somalia

Wapiganaji wa Al-shabaab
Image caption Wapiganaji wa Al-shabaab

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hisb al-Islam la Somalia, linasema limesitisha uhasama na kundi maarufu la Al-Shabaab.

Msemaji wa Hisb al-Islam, Mohamed Osman Arus, amesema kundi lake litavunjwa na wapiganaji wake kujiunga na kundi la Al-Shabaab linalodhibiti maeneo mengi kusini na kati mwa Somalia.

Al-Shabaab bado halijatoa taarifa kuhusu muungano huo kati ya mahasimu hao wawili.

Serikali ya mpito ya Somalia ambayo inapata usaidizi kutoka wanajeshi wa Umoja wa Afrika imesema kuwa muungano huo hautabadilisha azimio lake la kurejesha utulivu nchini humo.

Serikali inadhibiti eneo ndogo mjini Moghadishu.