David Beckham apewa tuzo ya mafanikio

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya England David Beckham, amepewa tuzo ya BBC ya mwanamichezo aliyepata mafanikio katika maisha yake.

Image caption David Beckham

Beckham mwenye umri wa miaka 35, amechezea England mechi nyingi kwa mafanikio na ameshinda Ligi Kuu ya England mara sita akiwa mchezaji na pia Ubingwa wa Ulaya na klabu ya Manchester United.

Ameshinda ligi ya Hispania akiwa na klabu ya Real Madrid, baada ya kuuzwa kwa paundi milioni 25 akitokea United, kabla hajajiunga na klabu ya Galaxy ya Los Angeles Galaxy na pia aliichezea kwa mkopo klabu ya AC Milan kwa miaka miwili.

Mwaka Beckham 2001 aliteuliwa kuwa mwanamichezo wa mwaka wa BBC.

Akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Sir Bobby Charton, Beckham alisema: "Nina furaha kupokea tuzo hii kutokana na kile ninachopenda kukifanya na ninapendelea kukifanya zaidi, nimefurahi sana."

Kupokea tuzo hii kutoka kwa Sir Bobby, ambaye alikuwepo wakati nikianza kucheza soka, niheshima kubwa."

Aliendelea kueleza,:Soka ni mchezo wa timu nzima. Bila timu na kuungwa mkono nilikokuwa nikipata kwa miaka yote hiyo, wachezaji kama Ryan Giggs na wengine wakubwa, nisingekuwepo hapa kama si wao kuniunga mkono na uwezo wao mkubwa wa kusakata soka."

"Kuichezea England ni moja ya mambo makubwa katika maisha yangu ya uchezaji soka, na kila mara nimekuwa nikicheza chini ya waalimu bora katika maisha yangu yote ya soka."

"Nawajibika kuwashukuru watu wengi, wazazi wangu, ambao walijitolea sana, ambao mara zote walifanya na wataendelea kufanya, familia yangu na rafiki na bila shaka mke wangu na watoto wangu. Mke wangu Victoria si tu kama amenipatia watoto watatu wazuri, lakini ameniunga mkono kila siku."