Majasusi wa Israel wanyongwa Iran

Maafisa wa serikali ya Iran wamesema watu wawili waliohukumiwa kifo kwa kosa la kuwa majasusi wa Israel nchini humo na kosa la kuwa na uhusiano na kundi la upinzani la People's Mujahedin, wamenyongwa.

Image caption Unyongaji Iran

Afisi ya kiongozi wa mashtaka mjini Tehran, imesema Ali Akbar Siadat alikuwa ametoa taarifa kwa idara ya ujasusi ya Israel, Mossad, kuhusu makombora pamoja na vituo vya kijeshi nchini Iran.

Mtu wa pili, Ali Saremi alikamatwa mwaka 2007 baada ya kuhudhuria sherehe za kuwaenzi wafungwa wa kisiasa.

Taarifa ya vyombo vya habari vya taifa nchini Iran, imesema Siadat alikiri kupokea dola elfu sitini kutoka Israel.

Hadi sasa serikali ya Israel haijasema lolote.

Ali Saremi, pia alituhumiwa kuwa na uhusiano na kundi la upinzani lililo ukimbizini la People's Mujahedin.