Marais watatu wa ECOWAS wapo I.Coast

Marais watatu wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi(ECOWAS) wamewasili nchini Ivory Coast katika kile kinachoelezwa hatua ya mwisho kumshawishi Rais Laurent Gbagbo, kuondoka madarakani kwa amani ama sivyo nguvu za kijeshi zitumike kumng'oa.

Image caption Laurent Gbagbo

Marais wa Sierra Leone, Cape Verde na Benin, watawasilisha waraka kutoka ECOWAS kwa Bw Gbagbo unaomtaka akubali ushindi wa Alassane Ouattara na kumkabithi madaraka.

Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Sierra Leone, Ibrahim Ben Kargbo, ameiambia BBC, marais hao waraka wao utakuwa bayana.