Raia wa Ivory Coast wapuuza kugoma

Wananchi wa Ivory Coast wameonekana kupuuza wito wa kushiriki mgomo wa kitaifa unaolenga kutatua mgogoro wa uchaguzi wa Urais uliofanyika nchini humo mwezi uliopita.

Image caption Alassane Ouattara

Mwandishi wa BBC katika mji mkuu Abidjan, amesema shughuli za kawaida zinaonekana kuendelea.

Vyama vya kisiasa vinavyomuunga mkono Alassane Ouattara, anayetambuliwa kimataifa ameshinda uchaguzi huo, viliitisha mgomo huo ili kujaribu kumlazimisha Rais wa sasa Laurent Gbagbo, aondoke madarakani.

Jumuiya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, Ecowas, imetishia kumchukulia hatua za kijeshi bw Gbagbo ikiwa hataondoka madarakani.