Wakimbizi wa Ivory Coast kusaidiwa

Mashirika ya misaada ya Msalaba Mwekundu na Mwezi Mwekundu yameanzisha wito wa kuchangisha dola milioni moja kusaidia nchi zinazopakana na Ivory Coast ili kusaidia watu wanaokimbia msukosuko wa kisiasa nchini humo.

Image caption Wakimbizi wa Ivory Coast katika kituo cha Msalaba Mwekundu

Liberia inajiandaa kupokea wakimbizi wapatao laki moja kutoka Ivory Coast.

Mapema, balozi mpya wa Ivory Coast katika Umoja wa Mataifa, alionya kuwa nchi hiyo inakaribia kuingia katika mauaji ya kimbari.

Balozi Yusufu Bamba, aliyeteuliwa na mtu anayedhaniwa kuwa mshindi na jumuiya ya kimataifa Alassane Ouattara, aliomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati suala hilo.

Rais aliyekuwa akitetea kiti chake Laurent Gbagbo amegoma kuachia madaraka.

Zaidi ya watu mia moja na sabini wamekufa katika ghasia tangu kufanyika kwa uchaguzi mwezi uliopita.