Mlipuko wa bomu wajeruhi saba Kigali

Watu saba, wakiwemo watoto, wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Image caption Ramani ya Rwanda

Polisi wamesema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili, wakati mtoto mwenye umri wa miaka 11, alipoliokota bomu hilo kando ya barabara.

Msemaji wa polisi alieleza majeruhi walipelekwa hospitalini na kutibiwa kwa majeraha madogo madogo waliyoyapata.

Alitoa wito kwa watu walio na silaha kinyume na sheria kuzisalimisha katika vituo vya polisi.

Waandishi wa habari wanasema mfuluflizo wa milipuko ya mabomu nchini Rwanda, mwaka jana ilisababisha vifo vya watu watatu na kuwajeruhi wengine kadha.