Ancelotti aona wingu zito kwa Chelsea

Meneja wa Chelsea, Carlo Ancelotti, anahisi nafasi ya timu yake kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya soka ya England, yanafifia baada ya kufungwa na bao 1-0 na Wolves.

Image caption Nafasi ya Chelsea yafifia

Bao la kujifunga mwenyewe la beki Jose Boswinga dakika ya tano, limewaacha mabingwa hao watetezi wakisota nafasi ya tano, wakizidiwa kwa pinti tisa na wanaoongoza ligi Manchester United.

Ancelotti amesema: "Ni vigumu kushinda ligi, lakini jambo lililo muhimu ni kurejea katika mstari wa ushindani na kucheza soka yetu, kupigana kiume na kusonga mbele."

Meneja Ancelotti aliongeza "bado nakabiliwa na chagizo, lakini sina wasiwasi na ajira yangu.

Chagizo inazidi kupanda kwa meneja huyo wa Chelsea, ambaye mwezi wa Oktoba alishuhudia timu yake ikipokonywa nafasi ya uongozi wa ligi, hali inayoashiria msimu ujao huenda wakapoteza nafasi ya kucheza mashindano ya Ubingwa wa vilabu vya Ulaya.