Dalglish akasirishwa na penalti ya Man U

Meneja wa Liverpool Kenny Dalglish, amemshutumu mwamuzi Howard Webb, baada ya kufungwa bao 1-0 na Manchester Unites siku ya Jumapili, katika mchezo wa raundi ya tatu wa kuwania Kombe la FA kwenye uwanja wa Old Trafford.

Image caption Kenny Dalglish

Webb aliipa Manchester United penalti baada ya Dimitar Berbatov kufanyiwa rafu na piam kadi nyekundu aliyomuonesha nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kwa kumchezea vibaya Michael Carrick.

"Ile penalti ilikuwa ni mzaha," alisema Dalglish. "Nimeangalia tena kwenye video na labda sheria ziwe zimebadilika, lakini ile haikuwa penalti.

"Na ile nyingine, Haikupaswa kuwa kadi nyekundu."

Dalglish, ambaye mara ya mwisho alikuwa meneja wa Liverpool mwaka 1991, alirejeshwa tena kuingoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu huu, kufuatia kutimuliwa kwa Roy Hodgson.

Kitu ambacho kilisisimua kurejea kwa Dalglish, ni mashabiki 9,000 wa Liverpool waliosafiri kwenda Old Trafford, ambao walionesha mapenzi makubwa kwake wakati wote wa dakika 90, tofauti na ilivyokuwa kwa Hodgson ambaye kwa kipindi chake cha miezi sita ya kuifundisha timu hiyo, hakupata mapenzi kama hayo

"Nadhani walicheza kwa kiwango kizuri na kupata matokeo yale katika mazingira magumu," Ameongeza Dalglish.