Manchester United yajishindilia kileleni

Manchester United imekwenda pointi tatu mbele zaidi na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England, baada ya kuwalaza Stoke City 2-1, katika uwanja wa Old Trafford, huku mshambuliaji Nani akiipatia timu hiyo ushindi huo muhimu.

Image caption Nani akiifungia bao la pili Manchester United dhidi ya Stoke

Bao la kwanza la Manchester United liliwekwa wavuni na Chicharito dakika ya 27, baada ya Berbatov kushindwa kutumia nafasi murua ya kufunga.

Nani, mshambuliaji machachari wa pembeni na mwenye kasi, aliihakikishia Man United pointi tatu muhimu kwa mkwaju mkali katika dakika ya 62 akijibu bao la kusawazisha la Stoke lililowekwa wavuni na Whitehead katika dakika ya 50.

Kwa ushindi huo Manchester United sasa wamezoa pointi 44 wakizidi kujishindilia kileleni.