Lionel Messi mchezaji bora wa dunia 2010

Shirikisho la Soka duniani, FIFA, limemtangaza mchezaji wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi, kuwa mchezaji bora wa soka wa mwaka 2010.

Image caption Lionel Messi

Hii ni mara ya pili mfululilizo kwa Messi, anayechezea klabu ya Hispania ya Barcelona, kupata tuzo hiyo.

Wachezaji wenzake wawili anaocheza nao katika klabu ya Barcelona, Xavi Hernandez na Andres Iniesta, pia walikuwemo katika kuwania tuzo hiyo.

Tuzo hiyo inapigiwa kura na makocha na manahodha wa timu, pamoja na waandishi wa habari waalikwa.

Jose Mourinho amechaguliwa kuwa kocha bora duniani kwa mwaka 2010 kutokana na jitahada zake za kubeba ubingwa wa Ulaya kwa vilabu, ubingwa wa Ligi ya Italia alipokuwa na klabu ya Inter Milan msimu uliopita.