Nigeria yatangaza kuimarisha ulinzi

Serikali ya Nigeria imetangaza mbinu mpya za kuimarisha usalama, kufuatia milipuko kadhaa ya mabomu usiku wa kuamkia sikukuu ya Krismasi na sikukuu ya mwaka mpya ambapo zaidi ya watu 80 waliuawa.

Image caption Hali baada ya shambulio Nigeria

Msemaji wa Serikali ya Nigeria, Ima Niboro, amesema Rais Goodluck Jonathan, atamteua mshauri maalumu juu ya maswala ya ugaidi na kuunda kamati za kupanga utaratibu wa umiliki na udhibiti wa milipuko na kuhamasisha raia juu ya hatari ya vitu hivyo.

Bwana Niboro pia alisema, Serikali itaweka kamera za televisheni, kuhakikisha kuwa watu aliowataja kama majambazi wa kisiasa, wanakamatwa na kushtakiwa haraka.