Waumini wa Coptic walalamika Misri

Waumini wa madhehebu ya Coptic nchini Misri, kwa mara ya pili wamepambana na maafisa wa usalama, huku malalamiko yakiendelea kufuatia waumini 21 kuuawa wakiwa kanisani kupitia mlipuko wa bomu, mjini Alexandria.

Image caption Hali nje ya kanisa lililoshambuliwa Alexandria

Mamia ya Wakristu waliandamana katika barabara za mji wa Alexandria, na katika mji mkuu wa Cairo, siku ya Jumapili.

Watu wachache wanahojiwa na polisi kuhusiana na mlipuko huo.

Hayo yakiendelea, kiongozi mmoja mkuu wa Waislamu nchini Misri, Sheikh Ahmed al-Tayeb, amemlaumu Papa Benedict kwa kuingilia masuala ya ndani ya Misri, wakati alipotoa wito kwa viongozi wa mataifa mbalimbali duniani, kuwalinda Wakristu wa Mashariki ya Kati.