Uandikishaji kura waanza Nigeria

Nigeria imeanza mchakato wa kuwasajili wapigaji kura, takriban milioni sabini, katika kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa Aprili mwaka huu.

Image caption Goodluck Jonathan, mgombea urais

Msemaji wa tume ya uchaguzi amesema kuwa shughuli hiyo, ya kuibuni orodha mpya, ilianza bila matatizo Jumamosi asubuhi.

Lakini baadhi ya wapigaji kura wamesema kuwa maafisa hawakuwepo katika baadhi ya vituo.

Shughuli za uchaguzi wa awali zilikumbwa na dosari baada ya majina ya baadhi ya wapigaji kura kukosekana.

Image caption Nuhu Ribadu, mgombea urais

Rais Goodluck Jonathan atawania Urais kupitia chama cha People's Democratic Party, na Nuhu Ribadu kugombea kiti hicho kupitia chama cha Action Congress.