Mauaji kwa risasi kisheria Somalia

Serikali ya Somalia imewauwa kwa kuwapiga risasi wanajeshi wake wawili na afisa mmoja wa polisi.

Image caption Wanajeshi wa Somalia

Haya ndio mauaji ya kwanza kutekelezwa na serikali tangu uongozi wa Siad Barre wa mwaka 1991.

Wanajeshi hao wawili na polisi mmoja waliuwawa kwa risai katika mji wa Mogadishu.

Walihukumiwa na mahakama ya kijeshi kwa kuwaua raia na wanajeshi.

Serikali ya mpito ya Somalia, ambayo inapata usaidizi wa jeshi la jumuiya ya Afrika, inadhibiti sehemu ndogo mjini Mogadishu