Gbagbo aamuru kufungwa kwa benki

Image caption Ivory Coast

Kiongozi wa Ivory Coast aliyepo madarakani Laurent Gbagbo ameamuru kufungwa kwa matawi ya benki kuu ya mataifa ya Afrika magharibi (BCEAO).

Mwandishi wa BBC John James huko Abidjan alisema kikosi cha polisi na magari yenye silaha yamezunguka makao makuu ya benki katika mji huo.

Benki hiyo ilimtambua mpinzani wa Gbagbo, Alassane Ouattara kama Rais baada ya uchaguzi wenye utata kufanyika mwezi Novemba.

Mwishoni mwa juma, gavana wa benki, ambaye ni mshirika wa Bw Gbagbo, alilazimishwa kujiuzulu na viongozi wa Afrika magharibi.

Mwandishi wetu alisema hatua hii ilimpa fursa Bw Ouattara kudhibiti fedha za taifa, ambaye aliamuru matawi yote kufungwa.

Ivory Coast ni sehemu ya nchi nane za Afrika magharibi inayotafiti fedha CFA, na benki moja ya kati mjini Dakar, Senegal, lakini ikiwa na makao makuu ya kitaifa katika kila nchi.