Jeshi Misri lasihi watu kurejea makwao

Jeshi nchini Misri limewataka waandamanaji kurejea makwao. Jeshi limetoa taarifa hiyo katika televisheni ya taifa, baada ya mapambano kati ya wafuasi wa Rais Hosni Mubarak na wale wa upinzani mjini Alexandria na maandamano mengine tofauti mjini Cairo.

Haki miliki ya picha g
Image caption Maandamano Misri

Mwandishi wa BBC katika eneo la Tahrir Square, amesema waandamanaji wanaendelea kukusanyika huku wengine wakimtaka Rais Hosni Mubarak asiondoke madarakani

mwezi Septemba kama alivyoahidi.

Kiongozi wa upinzani Mohamed ElBaradei amepuuza tangazo la Rais Hosni Mubarak kwamba ataondoka madarakani kipindi chake uongozini kikimalizika mwezi Septemba, akisema ni njia yake ya kusalia madarakani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mohamed ElBaradei

Siku ya Jumanne Rais wa Marekani Barack Obama, alitaka mageuzi yanayoendelea haraka nchini Misri yafanyike kwa njia ya amani.

Hata hivyo hakutoa wito wa kujiuzulu kwa Bw Mubarak ambayo ilikuwa sababu kuu ya maanadamano kwa wiki moja iliyopita.

Hata hivyo waandamanaji wameahidi kuendelea na maandamano na siku ya Jumatano asubuhi walijitokeza katika eneo la Tahrir kusisitiza Rais Hosni Mubarak aondoke madarakani.