Maandamano yafanyika Yemen

Maelfu ya watu wameandamana mjini Sanaa nchini Yemen.

Haki miliki ya picha none
Image caption Wafuasi na wapinzani wa serikali ya Yemen waandamana

Wapinzani na wafuasi wa rais Ali Abdullah Saleh waliandamana katika maeneo tofauti ya mji huo.

Mkutano wa upinzani uliendelea kwa saa chache lakini watu wanaoongoza maandamano walisema huu ni mwanzo tu.

Wapinzani wa rais Ali Abdullah Saleh wanataka mabadiliko ingawaje baadhi walisema hawataki kiongozi huyo kuondoka madarakani.

Rais Saleh amekuwa madarakani kwa miaka 32. Wafuasi wake walijitokeza mitaani mjini Sanaa wakisema pia wanataka mabadiliko chini ya uongozi wa rais Saleh.

Baada ya waandamanaji kuondoka, baadhi ya wanafunzi waliamua kubaki wakisema hawataondoka hadi pale rais Saleh atakapoondoka mamlakani.