Huwezi kusikiliza tena

Kisa na Mkasa na Salim Kikeke

Tembo na mwindaji

Mwindaji mmoja kutoka Poland ameishitaki kampuni moja ya utalii kwa kumpeleka mahala ambapo hakuna wanyama wa kuwinda.

Image caption Tembo

Shirika la habari la Reuters limesema majuzi Jumatano, kuwa kampuni hiyo ilimpeleka barani Afrika mwindaji huyo, kwa nia ya kwenda kuwinda tembo, lakini raia huyo wa Poland hakuona tembo hata mmoja.

Hata hivyo kampuni hiyo ya utalii iitwayo Jaworski Jagdreisen imesema mahala ilipompeleka mwindaji huyo nchini Zimbabwe, kuna wanyama.

"kwa kile ninachofahamu ni kuwa mwindaji huyo angeona hata kinyesi cha Tembo" amesema mmiliki wa kampuni hiyo.

Hata hivyo kampuni hiyo ilimuandalia tena mwindaji huyo, safari nyingine ya Afrika, na mara hii mwindaji huyo asiye na bahati alifanikiwa kupata tembo dume. Licha ya hivyo, mwindaji huyo ameendeleza kesi yake ya kudai fidia ya karibu dola laki moja na nusu. Kesi itasikilizwa februari 15.

Kanyonga mbwa

Haki miliki ya picha The Kennel Club Picture Library
Image caption Mbwa

Mamalaka nchini Marekani zimemshitaki mwanamama mmoja kwa kosa ya kutesa wanyama.

Mamlaka hizo zinadai mwanamama huyo Miriam Smith, alimnyonga mbwa mmoja kwa kumninginiza kwenye mti kwa kutumia waya, kwa sababu mbwa huyo alitafuta Biblia yake.

Maafisa wa wanyama wa Marekani wamesema siku ya Jumatatu kuwa, Bi Miriam, mwenye umri wa miaka 65, alimtundika mbwa huyo aliyejulikana kwa jina la Diamond, kwa sababu alikuwa na wasiwasi kwamba huenda angeweza kuwadhuru watoto wa majirani.

Mwanamama huyo wa Columbia, South Carolina alisema mbwa huyo ni shetani.

Mamlaka zinasema mabaki ya mbwa huyo yalipatikana yamefichwa kwenye majani, huku kipande cha waya kikiwa bado kwenye shingo ya mbwa huyo.

Mtandao wa Chinadaily.com umesema mwanamama huyo anakabiliwa na kifungo cha siku mia moja na themanini hadi miaka mitano jela, iwapo atakutwa na hatia.

Usiache chaja..

Polisi nchini Marekani, wamekamata bwana mmoja, aliyeacha simu yake ikichagi katika nyumba aliyoenda kuiba.

Image caption Mobile..

Kwa mujibu wa mtandao wa msn, mwizi huyo baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja huko Maryland, alipachika simu yake ukutani iendelee kuchaji, huku akikagua vyumba akitafuta vitu vya kuiba.

Kwa bahati mbaya au nzuri, mtoto wa mwenye nyumba hiyo alirudi nyumbani ghafla, na kumkurupusha mwizi huyo, aliyeruka kupitia dirishani na kukimbia.

Mtoto huyo aliita polisi, na walipopekua wakakuta simu ikiwa inachajiwa. Kwa kutumia mbinu za kipolisi, waliweza kumkamata mtu Cody Wilkins, ambaye baadaye alishitakiwa kwa makosa mengine kadhaa ya wizi.

Status ya Facebook

Polisi nchini Nigeria wanasema mtu mmoja ametupwa gerezani kwa kosa la kutoa laana kupitia ukurasa wake wa facebook kwenye mtandao wa internet.

Image caption Usokitabu

Mtandao wa habari wa Bulawayo news 24 umesema bwana huyo Moukhtar Aminu Ibrahim aliandika maneno yenye kumlaani gavana wa Nigeria Kaskazini.

Msemaji wa polisi wa Nigeria amesema bwana Aminu alikamatwa katika jimbo la Jigawa, kwa kumlaani Gavana Sule Lamido.

Katika ukurasa wake wa Facebook, Aminu aliandika "Mungu mlaani Sule Lamino na rafiki zake wote wasio na maana.

" Masemaji wa Lamido hakuweza kupatikana kuzungumzia jambo hilo ziku ya Jumatano. Kamata hiyo imekuja wakati Nigeria inakaribia kufanya uchaguzi wake wa uraia mwezi April.

Wizi mwingine

Bwana mmoja nchini Marekani ametupwa gerezani baada ya kuiba gari na kwenda kuiba benki, katika siku ambayo jaji alimuachilia huru ili asubiri hukumu ya kumpiga rafiki wake wa kike.

Image caption Dollar

Polisi wa Upper Yoda wamesema bwana huyo Richard Brandon Johnson mwenye umri wa miaka 29, alifanya wizi katika benki ya First Commonwealth, muda mfupi baada ya kufunguliwa siku ya Jumatano asubuhi.

Hata hivyo alikamatwa saa mbili baadaye, na kushitakiwa kwa kuiba gari, na kuiba benki.

Alishindwa kujiwekea dhamana ya dola laki tano, na hivyo kutupwa ndani.

Mtuhumiwa huyo aligoma kuzungumza lolote mbele ya waandishi wa habari, ingawa alizungumza maneno mawili tu -- Habari mama -- akimsalimia mama yake kupitia televisheni.

na kwa taarifa yako......Ni wanyama wawili tu wana uwezo wa kutazama nyuma bila kugeuza shingo, kasuku na sungura.

Tukutane wiki ijayo.... Panapo majaaliwa...

Taarifa kutoka mitandao mbalimbali ya habari