Watu wanne wameuwawa nchini Tunisia

Watu wasiopungua wanne wameuwawa nchini Tunisia, wakati polisi walipowafyatulia risasi waandamanaji, katika mji wa Kef, kaskazini mashariki mwa nchi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Maandamano Tunisia

Waandamanaji wawili waliuwawa kwenye maandamano, na wengine wawili wakafariki kutokana na majeraha wakiwa njiai kupelekwa hospitalini.

Maafisa waliwafyatulia risasi umati mkubwa wa waandamanaji waliokusanyika nje ya kituo cha Polisi na kuwasha moto, wakitaka mkuu wa kituo hicho kujiuzulu.

Imeripotiwa mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya kituo hicho cha Polisi mjini kef kufuatia taarifa kwamba kamanda wa polisi alimpiga kibao mwanamke mmoja, hatua iliyowakera zaidi, na wakawa wanajaribu kulivamia jengo hilo.

Tukio hili la nchini Tunisia linafuatia amri ya kutotoka nje iliyotangazwa na serikali baada ya maandamano yaliyomlazimisha Rais Ben Ali kuacha madaraka, na baadaye muda wa amri hiyo ukapunguzwa kwa saa mbili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanafunzi wa Tunisia waunga mkono raia wa Misri

Kuna mtazamo kuwa maandamno ya Tunisia yalichochea maandamano nchini Misri na nchi zingine za eneo la Uarabuni.