Lampard nahodha wa England

Frank Lampard wa Chelsea amepewa nafasi ya unahodha katika mechi ya kirafiki dhidi ya Denmark, Jumatano.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Frank Lampard

Lampard aliye na umri wa miaka 32 atachukua nafasi ya Rio Ferdinand na nahodha msaidizi Steven Gerrard ambao walijeruhiwa katika michuano ya klabu zao mwishoni mwa juma.

Aidha meneja wa Uingereza Fabio Capello amesema kuwa Jack Wilshere wa Arsenal ataichezea England kwa mara ya kwanza.

Image caption Bao la Lampard lililokataliwa Kombe la Dunia

'Najivunia sana, sikutaraji hivi,' alisema Lampard ambaye atakuwa nahodha wa timu ya Uingereza kwa mara ya kwanza.

'Nimekuwa katika timu hii kwa muda mrefu sana na najihisi kuwa mkongwe. Itakuwa nafasi ya kujivunia katika kazi yangu kuwaongoza vijana hawa,' aliongezea.

Image caption Frank Lampard

'Nitajaribu kufanya kama kile ninachoifanyia Chelsea. Sitabadilika kwa sababu ya kupewa cheo hicho. Timu huwa inahitaji viongozi na nitajaribu kadri niwezavyo katika utendaji kazi na kuleta hamasa kwenye timu.'

Lampard amechezea timu yake ya taifa mara 83 na kufunga magoli 20 lakini alijeruhiwa msimu uliopita akiwa na Chelsea na hajacheza mechi yoyote ya kimataifa baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya hungary mwezi wa Agosti.