Senegal yairarua Rwanda 2-0

Senegal ilianza vizuri kampeni ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika, kwa wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani 2011 (Chan) kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Rwanda.

Haki miliki ya picha bb
Image caption Senegal yaanza vizuri

Ushindi huo umeipeleka Senegal hadi kileleni mwa kundi la D, baada ya Angola na Tunisia kutoka sare ya 1-1 siku ya Jumatatu usiku.

Bao la kwanza la Senegal lilifungwa na Moustapha Kasse katika dakika ya 89.

Katika muda wa nyongeza kabla mpira haujamalizika, Mohamed Diop akaipatia Senegal bao la pili kwa mkwaju wa free-kick.

Kulikuwa na bao la dakika za mwisho pia katika mchezo wa pili.

Tunisia walikuwa wanadhani wamekwishapata pointi tatu kutokana na bao la moja lililofungwa na Youssef Msakni katika dakika ya saba ya mchezo.

Lakini katika dakika ya 92, Kali akaisawazishia Angola na kubadilisha upepo wa mchezo.