Wakili wa Taylor 'asusia' mahakama

Wakili wa Charles Taylor aliondoka kwa hasira mahakamani wakati kesi ya mtuhumiwa huyo, aliyekuwa Rais wa Liberia ikiendelea.

Image caption Wakili wa Taylor

Wakili huyo, Courtenay Griffiths, alikuwa akijaribu kuwasilisha maelezo ya mwisho mahakamani, siku ishirini baada ya muda wa kuwasilisha ombi lake kupita.

Alikasirika baada wa majaji wa mahakama hiyo kukataa ombi lake.

Uhalifu wa kivita

Bw Taylor anatuhumiwa kwa kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka wa 1990 na kuwasaidia waasi.

Alikana mashitaka kumi na moja dhidi yake ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kesi hiyo ilianza mwezi Juni 2007 na hukumu inatarajiwa baadaye mwaka huu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Charles Taylor

Waaendesha mashitaka waliendelea kutoa maelezo yao mwisho kwa mahakama hiyo licha ya Bw Griffiths' kutohudhuria kipindi cha mwisho katika kesi hiyo.

Akiwa nje ya mahakama hiyo Bw Griffiths alisema atapinga jinsi kesi itakavyoendeshwa.

Image caption Charles Taylor

Bw Griffiths aliongezea, "Uaminifu wa mahakama hii uko taabani kwa vizazi vijavyo ikiwa dakika ya mwisho wakati wanamzuia Bw Taylor kuwasislisha asilimia tisini 90% ya maelezo ya kufunga kesi hii".

Lakini mwendesha mashitaka Brenda Hollis amesema Bw Griffiths hakuwa na haki ya kuondoka anavyotaka.

Alisema, "Huu sio mkusanyiko wa kijamii na hawezi kuondoka tu dakika ya mwisho."

Waendesha mashitaka wamesema kuwa Bw Taylor, ambaye alikuwa Rais wa Liberia kati ya mwaka 1997 na 2003, aliwasaidia kwa kuwapa silaha waasi na kuongoza kundi la Revolutionary United Front(RUF) wakati wa utawala wa vitisho hususan dhidi ya raia.

Uhalifu

RUF ilileta hali ya wasiwasi kwa wananchi kwa kuwakata miguu na kufanya ubakaji kuwatisha wananchi.

Waendesha mashitaka walisema uhalifu uliotendwa kwa wananchi wa Sierra Leone usingetokea iwapo Bw Taylor asingekuwa mfadhili wa RUF.'

Lakini Bw Taylor alisema kuwa alikuwa akitaka kuleta amani Sierra Leone.

Image caption Charles Taylor

Anatuhumiwa kwa kuuza almasi na kuwapa silaha waasi

Mwaka jana, mwana mitindo Naomi Campbell na muigizaji Mia Farrow waliitwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Almasi

Waendesha mashitaka walikuwa wakijaribu kubaini uhusiano gani uliopo kati ya Bw Taylor na idadi ya almasi alizopewa Bi Campbell akiwa Afrika Kusini mwaka 1997.

Mahakama maalum inayoshughulikia kesi ya Sierra Leone huko The Hague Uholanzi imesikia mashahidi zaidi ya mia moja katika kesi ya kwanza inayomhusu Rais.

Image caption Taylor

Waendesha mashitaka watawasilisha maelezo yao ya kufunga kesi Jumanne, huku mawakili upande wa utetezi wakiwasilisha maelezo yao siku ya Jumatano na kukanusha mashtaka siku ya Ijumaa.

Hukumu inatarajiwa katikati ya mwaka 2011.

Iwapo atakutwa na hatia, Bw Taylor atafungwa nchini Uingereza.