Polisi Algeria wazuia maandamano

Maelfu ya maafisa wa usalama wamepelekwa katika mji mkuu wa Algeria, Algiers, kuzuia maandamano yaliyopangwa na wanaharakati wa demokrasia nchini humo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wa Algeria

Maandamano hayo yamekatazwa na serikali, japo makundi ya upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu wamesisitiza wataendelea na mipango yao wakidai kuneemeshwa kwa hali ya maisha na kupewa uhuru zaidi.

Siku ya Ijumaa polisi nchini Algeria walikuwa na wakati mgumu kuwazuia wananchi waliosherehekea katika barabara kuu za nchi hiyo, baada ya kutolewa habari za kujiuzulu Rais wa Misri Mohammed Hosni Mubarak.

Mwandishi wa BBC mjini Algiers anasema serikali hiyo inajaribu kuzuia mapinduzi kama yaliyofanyika nchini Misri na Tunisia.