Agizo latolewa Pervez Musharraf akamatwe

Mahakama ya kukabiliana na ufisadi nchini Pakistan inayoendesha uchunguzi dhidi ya mauaji ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benazir Bhutto, imetoa agizo la kukamatwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Pervez Musharraf.

Image caption Pervez Musharraf

Waendesha mashtaka wamesema Musharraf alijua njama za Taliban za kumuua Bi Bhutto, lakini hakutoa maelezo kwa idara zinazohusika za usalama.

Pia wamemshutumu kwa kutompa Waziri Mkuu huyo ulinzi wa kutosha.

Benaziri Bhutto aliuawa mwezi Disemba mwaka 2007alipokuwa akitoka na msafara wake katika maandamano ya kampeni za uchagzui.

Musharraf kwa upande wake amekanusha madai ya kuhusika kwa njia yoyote na mauaji ya Benazir Bhutto.