Waandamanaji waondoka mitaani Misri

Maelfu ya waandamanaji nchini Misri wameondoka katika eneo la wazi la Tahrir katika mji mkuu wa Cairo, baada ya utawala wa kijeshi kuahidi kuisitisha katiba ya nchi hiyo na kulivunja bunge.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mmoja wa waandamanaji akiwa Tahrir

Baraza kuu la kijeshi pia limesema litakaa madarakani kwa miezi sita, au hadi utakapofanyika uchaguzi.

Tangazo hilo limepokelewa vyema na waandamanaji wengi, wakiona kama kuvunjika kabisa kwa utawala uliopita, ingawa jeshi bado lijajitahidi kuondoa waandamanaji sugu katika eneo la Tahrir.

Rais wa Misri aliondka madarakani siku ya Ijumaa, baada ya siku 18 za maandamano.

Kwa siku ya pili mfululizo, polisi wa kijeshi walikuwa wakiwataka waandamanaji kadhaa waliosalia kuondoka katika eneo hilo. Baadhi yao wamesema wametishiwa kukamatwa iwapo hawataondoka.