KIZZA BESIGYE

KIZZA BESIGYE:

JINA: WARREN KIZZA BESIGYE KIFEFE

HADHI: KANALI MSTAAFU WA UPDF NA MWENYEKITI WA FORUM FOR DEMOCRATIC CHANGE –FDC.

MSHIKA BENDERA WA: INTER-PARTY COOPERATION-IPC

KUZALIWA: Rukungiri,Magharibi mwa Uganda.

TAREHE YA KUZALIWA: APRIL 22, 1956.

Kizza Besigye alizaliwa eneo la Rukungiri ,magharibi mwa Uganda.April 22,1956.Ni mtoto wa pili katika familia ya watoto sita.Alipata elimu ya msingi katika shule za Kinyasano na Mbarara Junior School.Wazazi wake waliaga dunia akiwa katika shule ya msingi.Alisomea katika shule za sekendari za Kitante High School huku kidato cha tano na sita alikuwa katika shule ya Kigezi High.Alijiunga na chuo kikuu cha Makerere kusomea udaktari 1975 na kufuzu kwa kupata shahada mwaka wa 1980.

Aliwahi kufanyia kazi Nairobi Kenya katika hospitali ya Aga Khan.Kutoka huko alijiunga na wapiganaji wa msituni wa National Resistance Army-NRA-kati ya 1980 – 1986.Wapiganaji hao walikuwa wakipinga utawala wa serikali ya Milton Obote.akiwa msituni miongoni alihusika na afya ya wapiganaji wa NRA.

Wakati Museveni aliposhika madaraka 1986,Besigye aliteuliwa kuwa waziri wan chi wa mamno ya ndani.Mnamo 1988 aliteuliwa kuwa waziri wan chi katika ofisi ya rais na pia na kuwa kamisa wa kitaifa wa masuala ya kisiasa yaani National Political Commissar.Mnamo 1991 aliteuliwa kuwa mkuu wa kikosi cha Mechanised Regiment eneo la Masaka, tena miaka mitatu baadae alikuwa mkuu wa vitendea kazi na uhandisi jeshini.Kabla ya uchaguzi mkuu wa 2001 alitoka jeshini akiwa na cheo cha Kanali.Besigye alioa Winnie Byanyima 1998 na wana mtoto wa kiume Anselm Besigye aliezaliwa Septemba 1999.

Besigye alishiriki katika uchaguzi mkuu wa 2001 kama mpinzani wa kiongozi wa sasa Yoweri Museveni.Museveni alishinda uchaguzi huo lakini besigye akapinga akidai kulifanyika mizengwe na kushtaki mahakamani.Besigye alishindwa mahakamani.

Mnamo juni 30, 2001, Besigye alikamatwa na kuhojiwa na kuhusu masuala ya usalitui.Septemba mwaka huo alitorka na kwenda uhamishoni nchini Marekani na baadae Afrika Kusini akisema kuwa maisha yake yalikuwa hatarini.

Besigye alirejea kutoka uhamishoni Oktoba 2005 kutoka uhamishoni na Novemba 14,2005, alishtakiwa kesi za uhaini baada ya kuhusishwa na makundi ya uasi ya Lord Resistance Army na Peoples Redemption Army na vilevile ubakaji wa mwana mke mmoja.

Katika uchaguzi mkuu wa 2006 chama cha Besigye cha Forum for Democratic Change-FDC-kilikuwa ndio chama kikuu cha upinzani na Besigye kama mpinzani mkuu dhidi ya Museveni katika uchaguzi mkuu wa urais mwaka huo.Matokeo yake yalimrejesha madarakani Museveni kwa kipindi kingine cha miaka mitano.Museveni alipata ushindi wa kura 59% dhidi ya Besigye 37% aliedai kutokea mizengwe.Baadae mahakama kuu ya Uganda iliamua kuwa uchaguzi ulijawana mizengwe hata hivyo mahakaam hiyo iliamua kuheshimu matokeo ya uchaguzi kwa kura 4-3.