Marekani yaunga maandamano nchini Iran

Maandamano ya raia nchini Iran Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano ya raia nchini Iran

Waziri wa Mashauri ya nchini za kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, amewapongeza waandamanaji wanaopinga serikali nchini Iran.

Waandamanaji hao wamekabiliana vikali na maafisa wa usalama katika mji mkuu wa Tehran huku maandamano hayo yakiendelea kuongezeka.

Bi Clinton, amesema maandamano hayo ni ushahidi kamili, juu ya ujasiri wa watu wa Iran, ambao kwa sasa wanakabiliana na serikali ambayo imekuwa ikiunga mkono maandamano nchini Misri, kutokana na unafiki wake.

Raia wa nchi hiyo wameandamana katika sehemu mbali mbali za mji mkuu wa wa Tehran na sehemu zingine nchini humo.

Shirika moja la habari la nchini Iran, limesema mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi katika machafuko hayo.