Chelsea yatolewa kombe la FA

Bingwa mtetezi Chelsea imetolewa katika raundi ya nne ya michuano ya kombe la FA, baada ya kufungwa na Everton kupitia mikwaju ya Penati.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Everton yaitoa Chelsea

Mpaka dakika 90 za mwanzo zikimalizika hakuna timu iliyokuwa imepata goli lolote na kulazimika kwenda dakika za nyongeza.

Chelsea wakicheza nyumbani walipata bao la kuongoza katika dakika ya 104 lililofungwa na Frank Lampard, lakini Leighton Baines alisawazisha bao hilo dakika moja kabla ya kupenga cha mwisho kupulizwa na kulazimika kupigwa penati.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Lampard wa Chelsea

Mkwaju wa Nicholas Anelka ulichezwa na kipa Tim Howard, wakati Ashley Cole alipiga nje. Penati ya Everton iliyochezwa na kipa Peter Chech ilipigwa na Leighton Baines.

Phil Neville ndio alipiga mkwaju wa ushindi wa Everton.

Everton sasa itakutana na Reading katika raundi ya tano.