Waandamanaji watawanywa Algeria

Polisi wa kutuliza fujo wamewatawanya waandamanaji mia kadhaa wanaoipinga serikali katika mji mkuu wa Algeria;Algiers.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wakiwatawanya waandamanaji Algeria

Waandamanaji hao walijaribu kuandamana mitaani lakini polisi waliwazuia kabla ya kukaribia kitovu cha jiji hilo.

Waandamanaji hao walipiga mekelele "uhuru na demokrasia kwa Algeria " na baadhi yao walichana picha za Rais , Abdul Aziz Bouteflika, ambae amekua madarakani tangu mwaka 1999.

Magari ya deraya yaliekwa katika maeneo muhimu ya mji na ndege za helikopta zilikua zikiruka angani. Polisi walimtia mbaroni Belayid Abrika mwanaharakati mashuhuri wa upinzani anaetetea haki za jamii ya Berber walio wachache nchini.

Naibu kiongozi wa kikundi cha upinzani kinachojiita umoja wa utamaduni na demokrasia , Tahar Besbas, alijeruhiwa alipopigwa na polisi. Maandamano hayo yalitayarishwa na vikundi vya kutetea haki za binaadamu,vyama vya wafanyikazi na muungano wa vyama vya kisiasa ingawa vyama vikuu vyaupinzani havikushiriki.