Ravalomanana azuiliwa kurudi Madagascar

Rais wa Madagascar aliyeondolewa madarakani Marc Ravalomanana anayeishi uhamshoni Afrika Kusini amezuiliwa kurudi nyumbani.

Image caption Aliyekuwa Rais wa Madagascar, Marc Ravalomanana

Bwana Ravalomana, aliyepinduliwa miaka miwili iliyopita anasema ameambiwa na Shirika la Ndege la Afrika Kusini kwamba yeye ni mtu asiyetakiwa nchini Madagascar.

Hapo awali alisema atarudi nyumbani leo kujaribu kumaliza mkwamo wa kisiasa wa hivi sasa, ingawa angeweza kukamatwa.

Bwana Ravalomanana alihukumiwa kifungo cha maisha nchini mwake kwa sababu ya waandamanaji waliouliwa na askari wa usalama.