Wamarekani watekwa nyara

Raia wanne wa Marekani waliokuwa wakisafiri karibu na mwambao wa Oman wameshikwa mateka na maharamia kutoka Somali.

Image caption Mharamia wa kisomali

Imeelezwa kuwa mashua hiyo S/V Quest ilikuwa ikielekea Oman kutoka India.

Maharamia huwa wanashambulia meli za bidhaa lakini katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakiziteka nyara mashua ndogo pia.

Ripoti kuhusu mashua ya S/V Quest ilitolewa na shirika la kimataifa linalohusika na maswala ya meli, pamoja na kikosi cha kupamabana na uharamia, Ocean Shield.

Wamiliki wa mashua hiyo Jean na Scott Adams, wamekuwa wakisafiri baharini tangu mwaka wa 2002 kulingana na tovuti yao.

Kwenye tovuti yao kuna habari kwamba walikuwa wameajiri mabaharia wawili mwaka jana.

Kadhalika walieleza kuhusu mipango yao ya kusafiri kwa mwaka huu kuondoka Sri Lanka kuelekea Crete kupitia mfereji wa Suez, na pia India, Oman na Djibouti katika msafara huo.