Mazungumzo kuanza Bahrain

Upande wa upinzani wa Bahrain unatarajiwa kukutana na mwana wa mfalme kufanya mazungumzo hii leo huku waandamanaji wanaendelea kuikalia medani kuu ya mjini Manama.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwana wa mfalme Bahrain, Salman bin Hamad Al-Khalifa

Hapo jana waandamanaji waliikalia Medani ya Lulu mjini Manama baada ya mwana wa mfalme, Sheikh Salman bin Hamad Al-Khalifa, kuwaamrisha wanajeshi na magari ya deraya kuondoka.

Mwandishi wa BBC alioko hapo anasema watu wako furahani katika medani hiyo.

Mfalme Hamad bin Isa Al-Khalifa amempa mtoto wake jukumu la kuanzisha mazungumzo na upinzani.

Waandamanaji wanadai mabadiliko ya amani ya kuleta demokrasi baada ya siku kadha za fujo ambapo watu waliuwawa katika mapambano na jeshi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji nchini Bahrain

Ripoti za hapo awali zilieleza kwamba kundi kuu la upinzani la wafuasi wa Kishia , Wefaq, lilikataa pendekezo la mfalme la kufanya mazungumzo ya kujaribu kukomesha machafuko yaliyoendelea kwa muda wa siku nane.

Kilidai kuondolewa kwa wanajeshi kutoka mitaani kabla ya kuanza mazungumzo yoyote.