Maelfu ya waandamanaji Rabat, Morocco

Maelfu ya waandamanaji wamejumuika mjini Rabat Morocco kudai kuwa Mfalme Mohammed,agawe sehemu ya madaraka yake.

Image caption Mfalme wa Morocco, Mohammed

Ripoti zinasema polisi wamesimama mbali na waandamanaji katika maandamanao yaliyoanzia kwenye mlango wa mji wa kale kuelekea majengo ya bunge.

Polisi hawakuwasumbua waandamanaji walipokuwa wakikaribia jengo la bunge wakiimba 'hatuitaki katiba ya utumwa'.

Kuna maandamano mjini Casablanca nchini humo na mengine yamepangwa kufanywa Marrakesh.

Maandamano ya Jumapili yalipangwa na makundi mbaliimbali ikiwemo kundi linaloijiita Kundi la mabadaliko ya Februari, "The February Movement for Change", ambao una mvuto kubwa zaidi kwenye mtandao wa kijamii wa intaneti, Facebook.

'Haya ni maandamano yasiyo na vurugu na ni ya kuishinikiza serikali ibadili katiba na kuwa inayoheshimu binadamu na kutokomeza ufisadi,' alisema Mustapha Muchtati kutoka kundi la Baraka, mojawapo ya makundi yanayoandaa maandamano hayo.

Waziri wa Fedha wa Morocco Selaheddine Mezouar amewahimiza raia kuacha maandamano, akisema kuwa endapo maandamano haya yatachochea vurugu zaidi nchi hii itapoteza utulivu na imani, tuliyojenga katika kipindi cha muongo moja, katika siku chache tu.'

Wadadisi wanasema, katika nchi za Kiarabu zilizokumbwa na maandamano ya raia, Morocco ni tofauti kwani ina uchumi uliostawi, wabunge waliochaguliwa na wananchi na ufalme unaoleta mabadiliko; kwa hivyo maandamano huko hayatoshika kasi.