6 wauwa katika vurugu Ivory Coast

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vurugu imekuwa ikishuhudiwa nchini Ivory Coast tangu mwaka uliopita.

Takriban watu sita wameripotiwa kufa nchini Ivory Coast Jumatatu iliyopita wakati wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji katika mji mkubwa zaidi, Abidjan.

Walioshuhudia wanasema wanajeshi watiifu kwa kiongozi aliye madarakani, Laurent Gbagbo, waliwapiga risasi wafuasi wa Alassane Ouattara, kiongozi wa upinzani anayetambulika na jamii ya kimataifa kama aliyeshinda uchaguzi wa urais wa mwaka uliopita.

Ujumbe wa Muungano wa Afrika unaozuru Ivory Coast unatarajiwa kurudia matakwa yao kumtaka Bw Gbagbo ajiuzulu.Ivory