Leyton kwenda Las Vegas kuibana Arsenal

Mwenyekiti wa klabu ya Leyton Orient Barry Hearn, atawapeleka wachezaji wake Las Vegas ikiwa ni zawadi ya kuwabana na kutoka sare ya 1-1 na Arsenal katika mchezo wa wa kuwania Kombe la FA.

Image caption Barry Hearn

Jonathan Tehoue aliisawazishia Leyton Orient katika dakika ya 89 na kuipatia timu hiyo inayocheza ligi ya daraja la pili nafasi ya mchezo wa marudio utakaochezwa uwanja wa Emirates.

"Wachezaji wa Leyton Orient walikuwa wakiimba wimbo maarufu wa Elvis Presley Viva Las Vegas, wakati mwenyekiti wao alipokuwa akiingia katika chumba chao cha kubadilishia nguo, alieleza meneja wa klabu Russell Slade.

"Mwishoni mwa mwezi wa Mei au Juni itakuwa muafaka kutembelea Las Vegas kwa siku tatu au nne."

Hearn akiwa mwenye furaha alitania asubuhi ya Jumatatu kwamba anataka anataka kwenda moja kwa moja Vegas baada ya mchezo wa Jumapili katika uwanja wa Brisbane Road, lakini Slade akataka waende mara moja.

"Bao la kusawazisha lilikuwa ni muhimu sana kwetu," alisema Hearn.

"Nilitaka twende siku ya Jumapili usiku, lakini haikuwezekana kwa vile tuna mchezo na Huddersfield siku ya Jumamosi na meneja amesema lazima azingatie masuala ya utaalamu.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alishuhudia timu yake ikiongoza kwa bao la Tomas Rosicky, lakini Tehoue akasawazisha kuihakikishia timu yake nafasi ya mchezo wa marudio.

"Tuliwaonesha ni timu bora eneo la Leyton," aliongeza Hearn.

"Mchezo wa marudio ni hazina kubwa ya kupata pesa nyingi na ukiwa katika ligi za chini unahitaji kupata zaidi ya kile unachotaka kupata.

Wenger amekiri alikuwa hajawahi kumsikia mshambuliaji Mfaransa wa Orient, Tehoue, lakini Slade amebainisha amekuwa akimtumia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kama mchezaji mwa kubadilisha matokeo ya mchezo.