Wachunguzi uchaguzi Uganda watofautiana

Wachunguzi wa nje wa uchaguzi mkuu wa Uganda uliofanyika wiki iliyopita wanaonekana kutofautiana kuhusu jinsi uchaguzi huo ulivyokwenda. Kuna wanaosema ulikuwa huru na haki wakati wengine wengine wanakataa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchaguzi Uganda

Ujumbe wa wachunguzi kutoka Umoja wa Afrika ulioko Uganda kwa ajili ya uchaguzi huo mkuu, unasema uchaguzi haukuwa wa haki.

Lakini wajumbe kutoka Afrika Mashariki, COMESA na IGAD wanasema kama walliona ulikuwa wa haki na huru.

Kuhusu madai ya ujumbe wa Umoja wa Afrika pamoja na Jumuiya Madola ya ama kutokuwepo usawa na vilevile kutotofautisha chama tawala na serikali na ama ugawaji wa pesa, msemaji wa serikali Kabakumba Matsiko amesema kuwa Rais analindwa na katiba na pia chama chake cha NRM kilimdhamini kwa kumpa pesa.