Arsenal yainyatia United kileleni

Arsenal imeisogelea Manchester United kileleni katika ligi kuu ya England, baada ya kuichapa Stoke City kwa bao 1-0.

Bao hilo pekee na la ushindi limefungwa na mlinzi Sebastien Squillaci katika dakika ya 8.

Image caption Squillaci

Hata hivyo ushindi huo umetiwa doa, kutokana na wasiwasi baada ya nahodha Cesc Fabregas na Theo Walcott wakitoka uwanjani kutokana na majeraha.

Walcott awali aligonga mwamba na shuti lake, kabla la Squillaci kupiga kichwa mpira wa krosi ya Niklas Bendtner.

Stoke walijaribu kujibu mashambulizi, lakini kipa Wijciech Szczesny alizuia mkwaju wa John Carew, kalba ya mkwaju mwingine wa Robert Huth kupita juu kidogo ya mwamba wa Gunners.

Kwa matokeo haya, Arsenal wako pointi moja tu nyuma ya United walio kileleni.