Congo yapongezwa kuwaathibu wanajeshi

Image caption Msemaji wa Ikulu ya White House

Marekani imeipongeza serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kuwatia hatiani wanajeshi 9, waliohusika katika ubakaji wanawake wengi katika eneo la Baraka, Mkoa wa Kivu mashariki mwa taifa hilo.

Msemaji wa serikali ya Marekani, PJ Crowley, amesema kifungo cha jela kwa wanajeshi hao kilichotolewa mapema wiki hii, ni hatua muhimu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi waliohusika katika ubakaji

Zaidi ya wanawake 60 walibakwa katika shambulio lililotokea katika mji wa Fizi, mapema mwaka huu.

Miongoni mwa wale waliopatikana na hatia ni afisa wa ngazi ya juu katika jeshi, Kanali Kibibi Mutware Daniel, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

Hii ni mara ya kwanza kwa kesi ya ubakaji dhidi ya kamada wa jeshi kufanikiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.