Matokeo ya uchaguzi yaidhinishwa Niger

Rais wa Niger akipiga kura Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Niger akipiga kura

Mahakama kuu nchini Niger, imeidhinisha matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais, uliofanyika mwezi uliopita.

Wagombeaji wawili waliopata idadi kubwa ya kura, katika awamu ya kwanza watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi huo utakaoandaliwa tarahe 12 mwezi ujao.

Wawili hao ni kiongozi wa upinzani, Mahamadou Issoufou na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Seini Oumarou.

Wandishi wa habari wanasema Bwana Oumarou, anapigwa upato kushinda uchaguzi huo wa urais licha ya kuwa alipata chini ya robo ya kura zote zilizopigwa katika duru ya kwanza.